2 Timotheo 2:1-7 (OTB)
1Kwa hiyo, mwanangu, jipatie nguvu katika neema iliyo katika Kristo Yesu. 2Na yale uliyoyasikia kutoka kwangu mbele ya mashahidi wengi, wakabidhi kwa watu waaminifu ambao wataweza kuwafundisha wengine pia. 3Shiriki taabu pamoja nami, kama askari mwaminifu wa Kristo Yesu. 4Hakuna askari anayehudumu kwa bidii anayejishughulisha na mambo ya maisha ya kila siku, ili apate kumpendeza yule aliyemwandika. 5Na mtu akishindana kama mwanariadha, hapewi taji la ushindi isipokuwa akishindana kwa kufuata sheria. 6Mkulima mwenye bidii anapaswa kuwa wa kwanza kushiriki katika mavuno. 7Fikiri juu ya hayo nisemayo, na Bwana atakupa ufahamu katika mambo yote.
Fungua katika kisoma Biblia ↗